}

NYUMBA ZA MADANGURO UWANJA WA FISI KUBOMOLEWA.


Dar mpya inawezekana ikiwa kila mmoja wetu na kwa pamoja tuta shikamana kwa kufanya Kazi kwa bidii kila mtu katika nafasi yake ,lakini sikwa ulevi wala wala kuendesha biashara haramu.



Nibaadhi ya maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh Paul makonda , aliyo yasena wakati  alipo tembelea uwanja wa fisi tandale ambapo alikutana na baadhi ya nyumba zina  endesha biasha ya madanguro  akiwa ame  ambatana na Mkuu wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Kamishina Simon Sirro,na RPC wa Kinondon Suzana kaganda na waandishi wa habari.



Makonda alilazimika kugonga mlango  katika moja ya nyumba zinazo sadikiwa kuwa ni  ni danguro lakini watu walio kuwemo humo waligoma kufungua mlango .




Katika eneo hilo pia kulikuwa na watu wakinnywa pombe za kienyeji ambapo hali ya watu hao ili kuwa mbaya akalazimika kuuliza maswali ya kuwapima ufahamu "we we Rais wa Tanzania ninani? majibu  ni Nyerere  ,ni ....mimi.


Halihiyo imemlazimu  Mkuu wa Mkoa kuagiza eneo hilo kubomolewa na kuendelezwa kwa ajili ya uwekezaji  ili kukomeaha biashara hiyo haramu, Sikh chache zilizo pita Mkuu wa wilaya ya kinondoni  mh Alli Hapi alitangangaza eneo hilo kuwa lita kuwa la uwekezaji.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.